Awali Simba ilikaribia kumsajili mlinda lango kutoka Brazil Caique Luiz Santos hata hivyo ilisitisha mpango huo baada ya kubaini golikipa huyo anafahanmu lugha moja tu, Kireno
Manula atarejea uwanjani katikati ya mwezi Oktoba pale atakapokuwa amepona majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini
Katika wiki hii Simba inatarajiwa kufunga hesabu za usajili kwa kumtambulisha mlinda lango ambaye anatua kusaidiana na Ali Salim wakati Aishi Manula akiendelea kuuguza majeraha
Ni wazi angekabiliwa na changamoto katika kuwasiliana na wenzake hasa ikizingatiwa katika ukanda wetu lugha ya kireno sio miongoni mwa lugha zinazozungumzwa na wengi
Simba inatajwa kumuwania mlinda lango raia wa Cameroon Simon Omossola kutoka Fc Lupopo
Omosolla mwenye umri wa miaka 25 pia amewahi kuitumikia klabu ya AS Vita ya DR Congo hivyo ni mlinda lango ambaye ana uzoefu mkubwa katika mashindano ya CAF
Viongozi wa Simba wako kwenye presha kubwa ya kuhakikisha wanakamilisha dili la golikipa haraka ili apate nafasi ya kushiriki pre-season na wenzake huko Uturuki
No comments:
Post a Comment