Privacy policy

Privacy Policy
Updated at 2023-12-21
Tat ("we," "our or "us") is committed to
protecting your privacy. This Privacy Policy
explains how your personal information is
collected, used, and disclosed by Tat.
This Privacy Policy applies to our website,
htp://yangavideo.blogspot.com/2023/01/tod-
10ya-waigizajiwarembo-zaidi.html, and
its associated subdomains (collectively,
our "Service"). By accessing or using our
Service, you signify that you have read,
understood, and agree to our collection,
storage, use, and disclosure of your
personal information as described in this
Privacy Policy and our Terms of Service.
Definitions and key
terms
To help explain things as clearly as
possible in this Privacy Policy, every time
any of these terms are referenced, are
strictly defined as:

or are under contract to perform a service on behalf of one of the parties.
any information that directly, indirectly, or in connection with other information — including a personal identification number — allows for the identification or identifiability of a natural person.
refers to the service provided by
as described in the relative terms (if available) and on this platform.
Third-party service:
refers to advertisers, contest sponsors, promotional and marketing partners, and others who provide our content or whose products or services we think may interest you.
Website:
Tat
’s site, which can be accessed via this URL:
http://yangavideo.blogspot.com/2023/01/top-10-ya-waigizaji-warembo-zaidi.html.

MTENDA HUTENDWA


 
    ⚽Klabu ya Westham United 🔨 inahaha kutafuta mrithi wa kiungo wao ghali aliyetimkia kwa majirani zao wa jiji la London Arsenal kwa uhamisho wa paund 105£ Decline rice.
  >>Ambapo wagonga nyundo hao wamepeleka ofa kwa Mashetani wekundu👺 wenye maskani yao Old traford yenye thamani ya paund 35£ na ongezeko la 5£ ili kuinasa saini ya kiungo Scott Mctominay lakini wababe hao wa old traford wameendela kushikilia bomba kwa kusisitiza kua kiungo wao huyo raia wa scotland hauzi chini ya £45.

WANANCHIIII!!!! MWAMBA HUYU HAPA💛💚.



 Anaitwa Emmanuel Mahop(28) raia wa Cameroon anatajwa kuja kuvaa viatu vya mabingwa wa nchini Tanzania Yanga sc ambapo vyanzo vinasema hivi sasa wapo mjini Dar es salaam kwa ajili ya kukamilisha swala kutangazwa na kuanza majukumu yake mapya kma mwananchi ikumbukwe Mahop raia wa Cameroon ameshaaga katika timu aliokua akicheza awali.
📌 Emmanuel mahop takwimu zake misimu mitatu nyuma ni kama zifuatazo;
    🔒Nchini Guinea ligi daraja la pili 2020/21
        Mechi (15)
        ⚽- 30
        🎯- 4
    🔒Fc Akonagui  2021/22
        Mechi (22)
        ⚽- 15
        🎯- 5
    🔒Canone Younde 2022/23
         Mechi (20)
         ⚽- 15
         🎯- 3
  📌 Ambapo msimu huo alimaliza akiwa mfungaji bora na kubeba taji la ligi.

AS VITA KUMINYANA NA YANGA



Klabu ya As vita ya nchini DRC congo imejikita kambi nchini Tanzania kwa maandalizi ya msimu ujao wa mashindano wa 2023/24 nchini kwao Congo huku timu hiyo ikitarajiwa kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya mabigwa wa NBC Premier league Young Africans.

WAPI HATIMA YA MBAPE


MGUU WA KUTOKA 
Je vilabu ya ulaya vitafikia dau la al Hilal ya Saudi pro league 
@chelseafc 
@manchesterunited 
@spursofficial 
@realmadrid 
@alhilal

SAKHO KUKIPIGA UFARANSA


Klabu ya simba inatarajia kukosa huduma ya kiungo mshambuliaji wao raia wa senegal Pape Ousman Sakho baada ya kutua nchini Ufaransa kwa ajili ya kumaliza taratibu zake za usajili na Quevilly Metropelo Fc timu inayoshiriki katika daraja la pili nchini humo. 

ATATANGAZWA LEO?

Jezi namba sita imekuwa maarufu sana, ule wakati wa kumfahamu muhusika wake umefika!
Ni suala la muda tu Yanga itamtangaza mchezaji aliye nyuma ya jezi hiyo ambaye atakuwa 'surprise' kubwa kwa mashabiki

Hatakuwa peke yake! kwani Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe amebainisha kuwa kuna nyota wanne ambao watawatangaza wiki hii na Jumamosi Wananchi watawashuhudia pale uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs

Lakini gumzo zaidi ni jezi namba sita je ni nani? Wakati huu imekuwa sio rahisi kwa mchezaji huyo kufahamika! 

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe jana aliweka video ikimuonyesha Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akichora sura ya mchezaji huyo na kuwataka mashabiki wakisie anaweza kuwa nani?

KIPA KUTAMBULISHWA

Awali Simba ilikaribia kumsajili mlinda lango kutoka Brazil Caique Luiz Santos hata hivyo ilisitisha mpango huo baada ya kubaini golikipa huyo anafahanmu lugha moja tu, Kireno

Manula atarejea uwanjani katikati ya mwezi Oktoba pale atakapokuwa amepona majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji Afrika Kusini
Katika wiki hii Simba inatarajiwa kufunga hesabu za usajili kwa kumtambulisha mlinda lango ambaye anatua kusaidiana na Ali Salim wakati Aishi Manula akiendelea kuuguza majeraha
Ni wazi angekabiliwa na changamoto katika kuwasiliana na wenzake hasa ikizingatiwa katika ukanda wetu lugha ya kireno sio miongoni mwa lugha zinazozungumzwa na wengi

Simba inatajwa kumuwania mlinda lango raia wa Cameroon Simon Omossola kutoka Fc Lupopo
Omosolla mwenye umri wa miaka 25 pia amewahi kuitumikia klabu ya AS Vita ya DR Congo hivyo ni mlinda lango ambaye ana uzoefu mkubwa katika mashindano ya CAF

Viongozi wa Simba wako kwenye presha kubwa ya kuhakikisha wanakamilisha dili la golikipa haraka ili apate nafasi ya kushiriki pre-season na wenzake huko Uturuki

SAFARI UTAMBURISHO WA JEZI YAANZA

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Ahmed Ally ataongoza msafara wa maafisa wa klabu hiyo pamoja na Mdhamini wa jezi Sandaland The Only One kupanda mlinda Kilimanjaro kwa ajili ya uzinduzi wa jezi za klabu ya Simba 2023/24

Safari ya kupanda mlinda Kilimanjaro itaanza kesho Jumatano na msafara huo utafika kileleni siku ya Ijumaa, na kufanya uzinduzi wa jezi majira ya saa 1 usiku

Ahmed amesema tukio la Simba kuzindua jezi juu ya mlima Kilimanjaro lina baraka ya Mamlaka zote na Dunia nzima itashuhudia

KARIBU YANGA 🟢🟡✅



Karibu Jangwani Yao Kouassi 
Sio tetesi tena, sasa ni rasmi Yanga imekamilisha usajili wa mlinzi mahiri wa kulia Yao Kouassi Attohoula.

Mabingwa wa nchi wamemn'goa Yao Kouassi kutoka klabu ya Asec Mimosas ya Ivovy Coast
Kouassi ni mchezaji kiraka ambaye anaweza kutumika katika nafasi zote za ulinzi na hata kiungo mkabaji.

Kwa hakika Yanga imedhamiria kutetea makombe yote, usajili huu unatoa picha halisi ya mipango ya Yanga kuelekea msimu ujao.

Manara , Ali kamwe wahusishwa 'wameanza na hasara'


 

Mshery kupelekwa Tunisia


 KIPA wa Yanga, Abuutwalib Mshery yupo nje kutokana na jeraha la goti, lakini mabosi wa klabu hiyo wamepanga kumpeleka Tunisia ili kufanyiwa upasuaji na kuruhusu areje mapema uwanjani.

Mshery aliumia goti hali iliyowafanya mabosi wa Yanga kwenye dirisha dogo la usajili  kumrejesha kwa mkopo Metacha Mnata kutoka Singida Big Stars ili kuziba nafasi yake na Mwanaspoti limedokezwa kwamba kipa huyo yupo mbioni kuondoka kwenda Tunisia  kwa matibabu zaidi.
Inaelezwa Mshery atapelekwa hospitali aliyofanyiwa upasuaji Yacouba Songne na Kibwana Shomary ambao walirejea mapema uwanjani na Daktari wa timu hiyo, Youssef Ammar ili kuthibitisha taarifa hizo alikiri kuwa na mpango wa Mshery kupata matibabu nje ya nchi.
"Kweli atafanyiwa matibabu yake nje ya nchi kule Tunisia wakati timu ikiwa inaenda kucheza mechi yake dhidi ya US Monastir," alisema kwa kifupi Ammar.
Yanga itaondoka nchini Jumanne ijayo kwa ajili ya kuwahi mchezo wa kundi D wa Kombe la  Shirikisho Afrika dhidi ya US Monastir ya Tunisia utakaochezwa Februari 12 kisha ikirejea nchini itakuwa na mchezo dhidi ya TP Mazembe na baadae kuifuata Real Bamako ya Mali.
Kipa huyo alisaini mkataba wa miaka mitatu kuitumikia Yanga baada ya kufanya vizuri akiwa na kikosi cha Mtibwa Sugar.


Simba, Al Hilal hakuna mbabe


 MABINGWA wa Sudan Klabu ya Al Hilal wamelazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Simba katika mchezo mkali wa kirafiki wa Kimataifa uliochezwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.


Al Hilal ilikuwa ya kwanza kupata bao kupitia kwa nyota wake, Makabi Lilepo dakika ya sita tu ya mchezo huku Habib Kyombo akaiandikia Simba bao la kusawazisha dakika ya 81 kipindi cha pili.

Al Hilal iliwasili nchini Jumatatu ya Januari 25 kwa mwaliko maalumu wa Simba ikiwa ni sehemu ya makubaliano ya kimkataba baina ya timu hizo zinazojiandaa na Ligi ya Mabingwa Barani Afrika.



Mchezo wake wa kwanza tangu ilipowasili ililazimishwa sare ya bao 1-1 na Namungo FC Januari 26, katika mechi iliyokuwa kali na ya kusisimua iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex Chamazi.

Baada ya hapo Al Hilal iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC katika mchezo wake wa pili wa kirafiki uliochezwa Januari 31 Uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.

Miamba hii ya Sudan inakumbukwa zaidi na Watanzania kwani ndio timu iliyoiondosha Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika kufuatia kuifunga jumla ya mabao 2-1 kwenye hatua ya pili ya mtoano.

Baada ya mchezo huu Simba itasafiri hadi nchini Guinea kuanza safari yake ya matumaini katika hatua za makundi za Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza na Horoya, mechi itakayochezwa Februari 11.

Kwa upande wa Al Hilal nao wanakabiliwa na kibarua kizito Februari 11 wakati watakapoanza pia safari ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kucheza na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Simba iko kundi C sawa na timu za Raja Casablanca (Morocco), Horoya (Guinea) na Vipers ya Uganda huku Al Hilal iko kundi B na Al Ahly (Misri), Mamelodi Sundown (Afrika Kusini) na Coton Sport ya Cameroon.

Gael, Yanga ngoma mbichi

 


KIUNGO Mrundi Gael Bigirmana ameikalia kooni Yanga akitaka impe barua ya kuondoka na kumlipa mamilioni ya pesa baada ya kile alichodai kukiukwa kwa vipengele vya mkataba.


Sakata la mchezaji huyo lilianza usajili wa dirisha dogo ulilofungwa Januari 15, mwaka huu, ambapo Yanga ilimnyofoa Ligi Kuu na nafasi yake kumpa beki Mmali Mamadou Doumbia na kutimiza majina 12 ya mastaa wa kigeni.

Hata hivyo, Yanga ilimbakisha Gael kwenye usajili wa CAF, jambo ambalo kwa mujibu wa mmoja ya vigogo wa timu hiyo (jina tunalo), bado ni mchezaji wao kwani nyota huyo wa zamani wa Newcastle United ya Ligi Kuu England alisaini mkataba wa miaka miwili mwanzoni mwa msimu huu.



Suala hilo lilimlazimu Wakala wa Gael, Costantine Mutima kutoka England anakoishi kuja kuongea na viongozi wa Yanga akitaka maelezo ya kina lakini hadi sasa hakuna kilichoeleweka.

Mutima alizungumza na Rais wa timu hiyo, Hersi Said na Mtendaji Mkuu, Andrew Mtine ili kumaliza jambo hilo lakini inaelezwa mazungumzo hayakuwa na majibu ya moja kwa moja baada ya wakala huyo kutaka Yanga imlipe Gael asepe zake.

Inaelezwa Yanga iliendelea kutotoa ushirikiano wa kutosha kwa wakala huyo aliyekuwa amepanga kuondoka nchini na mchezaji wake mwanzoni mwa wiki hii, ndipo akaamua kuandika barua TFF akitaka uthibitisho wa usajili wa Gael kisha afuate hatua za kisheria ikiwemo kwenda Fifa.

Mwanaspoti linajua Gael ameingiziwa mshahara wa Januari na Yanga na bado yupo nchini akitarajia kuondoka siku yoyote kuanzia Jumatatu ijayo.

Mutima alipotafutwa kuzungumzia sakata hilo alisema Yanga haijampa jibu la moja kwa moja na muda unaenda kwani mteja wake hana furaha kikosini hapo.

“Ni kweli tumewaandikia TFF tukitaka watupe uthibitisho wa usajili na baada ya hapo tutafuata hatua nyingine za kisheria,” alisema.

Matola atumiwa nauli aingia mitini


MOJA ya makocha chipukizi wazawa ambao wanaaminika kuwa ni bora kwenye soka la Tanzania kwa sasa basi ni kocha msaidizi wa Simba Suleiman Matola ambaye amefanya mambo makubwa kadhaa kwenye soka la Tanzania.


Matola ambaye aliweka baadhi ya rekodi akiwa na Lipuli ya Iringa sehemu ambayo alitambulika sana, lakini pia akawa na Polisi Tanzania na kufanya tena mambo makubwa akiwa na Simba, siyo jina geni sana baada ya kukaa pia kwenye kikosi cha Simba kwa muda mrefu.



Amepitia mambo mengi akiwa na Simba, kuna wakati ameonja joto ya jiwe kutoka kwa mashabiki, kuna wakati ameshangiliwa na mashabiki haohao, hawa ndiyo watu wa soka, lakini katika maisha ya soka, Matola ana mambo mengi ambayo wengi hawayajui kwa kuwa siyo muongeaji sana na mara nyingi imekuwa ikielezwa kuwa ni mtu msiri sana kuhusu maisha yake ya nyuma ya soka.