Jezi namba sita imekuwa maarufu sana, ule wakati wa kumfahamu muhusika wake umefika!
Ni suala la muda tu Yanga itamtangaza mchezaji aliye nyuma ya jezi hiyo ambaye atakuwa 'surprise' kubwa kwa mashabiki
Hatakuwa peke yake! kwani Afisa habari wa Yanga Ali Kamwe amebainisha kuwa kuna nyota wanne ambao watawatangaza wiki hii na Jumamosi Wananchi watawashuhudia pale uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa kilele cha wiki ya Mwananchi dhidi ya Kaizer Chiefs
Lakini gumzo zaidi ni jezi namba sita je ni nani? Wakati huu imekuwa sio rahisi kwa mchezaji huyo kufahamika!
Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Instagram, Afisa Habari wa Yanga Ali Kamwe jana aliweka video ikimuonyesha Rais wa Yanga Injinia Hersi Said akichora sura ya mchezaji huyo na kuwataka mashabiki wakisie anaweza kuwa nani?
No comments:
Post a Comment